Dhima ya Nafasi
TEF Consult inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa, uwezo na ari ya kufanya kazi katika nafasi ya Key Account Executive (KAE) katika Kitengo cha Mauzo.
Taarifa za Nafasi
Nafasi: Key Account Executive (KAE)
Kitengo: Mauzo
Idadi ya Nafasi: Watu 50
Eneo la Kazi: Dar es Salaam
Kutoa na kusimamia huduma za Lipa kwa Simu / Lipa Namba kwa wafanyabiashara wakubwa na wa kati, kuhakikisha huduma zilizosajiliwa zinafanya kazi ipasavyo, kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara pamoja na kuchangia ukuaji wa mauzo.
Vigezo vya Mwombaji
Mwombaji anatakiwa:
- Awe na Diploma au Shahada katika Mauzo, Biashara, Usimamizi wa Biashara au fani nyingine inayohusiana na masuala ya mauzo.
- Awe na uzoefu katika shughuli za mauzo.
- Awe na uwezo wa kujisimamia na kufanya kazi kwa weledi.
- Awe mwenye nidhamu, bidii na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wateja.
- Awe na uwezo wa kutumia kompyuta.
- Awe tayari kufanya kazi kwa malengo na kufikia viwango vya mauzo vilivyowekwa.
Majukumu Makuu
- Kutoa huduma za Lipa kwa Simu / Lipa Namba kwa wafanyabiashara wakubwa na wa kati.
- Kuhakikisha huduma za Lipa kwa Simu/Lipa Namba zilizosajiliwa zinafanya kazi ipasavyo kwa wafanyabiashara.
- Kujenga na kudumisha ushirikiano mzuri kati ya wafanyabiashara na kampuni.
- Kufuatilia na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wanaotumia huduma hizo.
- Kuchangia katika kuongeza matumizi ya huduma na kufikia malengo ya mauzo ya kampuni.
- Kutoa huduma bora na msaada unaohitajika kwa wafanyabiashara.
Malipo
- Fixed Allowance
- Commission Based
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wenye sifa wanakaribishwa kutuma Wasifu (CV) kupitia mawasiliano yafuatayo:
Project Manager: Johanes Wambura
Simu / WhatsApp: 0675 467 878
Barua pepe: wambura@tefconsult.co.tz
Au
Online Application:
- Location
- Dar es salaam, tanzania
- Job type
- Part Time
Apply for this position
Complete your profile and attach clear, readable documents. Your application is saved privately and can only be reviewed by authorized recruitment staff.